Ijumaa, 6 Desemba 2013

MANDELA AKUTWA NA UMAUTI USIKU HUU:


RAIS wa kwanza wa Afrika Kusini na mpinga
siasa za ubaguzi wa rangi, Nelson Mandela
amefariki nchini humo akiwa na umri wa
miaka 95.
Taarifa za kifo chake zimetangazwa na rais
wa nchi hiyo, Jacob Zuma ambaye amesema
Mandela amefariki majira ya saa 2.50 usiku
wa Alhamisi kwa saa za Afrika Kusini.
Mandela amekuwa akisumbuliwa na maradhi
kwenye mapafu kwa muda mrefu, alilazwa na
baadaye kuruhusiwa kutoka hospitali ambapo
mauti yamemkuta akiwa nyumbani kwake
mjini Pretoria.
Tayari viongozi mbalimbali duaniani
wameshaanza kutuma salamu za rambirambi
kwa familia na taifa la Afrika Kusini.
Viongozi hao ni pamoja na Rais Barack Obama
wa Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa (UN), Ban Ki-Moon.














































































Alhamisi, 5 Desemba 2013

NELSON ‘MADIBA’ MANDELA BADO NI MAHUTUTI :


Haya ndiyo maneno aliyosema Binti wa aliyekuwa Rais wa kwanza mwafrika wa Afika Kusini, Makaziwe Mandela, alipokuwa anaeleza kuhusu hali ya Baba yake :

“…… Tunaendelea kumshukuru MUNGU kwa uwepo wa Baba hadi leo. Ni kweli anaumwa, anaumwa sana. Hata hivyo ukimwangalia bado unamwona mtu jasiri na mpambanaji. Anaonekana wazi ana maumivu makali lakini anajitahidi kutowaumiza walio karibu yake kwa kutokuonyesha wazi.

“…… Hata wakati huu akiwa kwenye kitanda chake cha mateso ya kuugua … tunaendelea kujifunza jambo kutoka kwake … upendo na uvumilivu. Tunawaomba watu wote waungane nasi kumwombea Mzee Mandela.”