Jumamosi, 30 Novemba 2013

MAAMBUKIZO YA UKIMWI YAONGEZEKA ZANZIBAR:


Zanzibar,
Mkurugenzi Mtendaji wa Kamishina ya Ukimwi Zanzibar (ZAC) Dk. Omar Shauri Makame amesema kwamba RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein atakuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yatakayofanyika Paje Mkoa wa Kusini Unguja .

Akitoa taarifa hiyo, Dk. Makame amesema maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika wakati kunaonekana kuwapo na ongezeko la maambukizi mapya.

Alisema katika mwaka 2012-2013 watu 108 walikutwa na maambukizi mapya na kufanya idadi ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi kufikia 6,125 kwa mujibu wa takwimu za watu waliofika katika vituo vya afya kuchunguza afya zao ikiwemo damu.

“Utafiti wa takwimu za ugonjwa wa Ukimwi zinaonesha kwamba yapo maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa kiwango kikubwa ambapo juhudi za makusudi zinahitajika.

“Kwa mfano alisema Tume ya Ukimwi imeweka mikakati kuyadhibiti makundi hatarishi ikiwemo vijana wanaotumia dawa za kulevya ambapo maambukizi ya kundi hilo yapo kwa asilimia 25’” alisema Dk. Makame.


Picha ni Ramani ya kisiwa cha Zanzibar ambacho ni maarufu kwa jina la marashi ya Karafuu.

Maoni 2 :

  1. hicho ni kisiwa cha unguja ambacho ni maarufu kwa utalii sio karafuu.

    JibuFuta
  2. kisiwa cha pemba ndo maarufu kwa marashi ya karafuu.

    JibuFuta