Kitunguu saumu kina harufu ya pekee isiyowapendeza watu wengi, ila kina
uwezo wa kutibu magonjwa lukuki ambayo na imani hukulijua hilo. Katika
nyakati hizi dunia yetu imezungukwa na magonjwa mengi ya maambukizi na
ya sio maambukizi kama mifupa, uchovu wa mwili na kadhalika.
Imethibitishwa kisayansi kuwa kitunguu saumu husafisha damu kutokana na
mafuta (cholestrol) ambayo husababisha magonjwa ya mishipa ya ateri na
maradhi ya moyo, na pia husafisha damu kutokana na vijidudu na
maikrobati kuliko (antibiotic) vengine. Sio hivyo tu bali kitunguu saumu
kimethibitika kuwa na uwezo wa kuzuia kuenea kwa sumu ya nyoka katika
mwili wa binadamu na husafisha maida kutokana na vimelea (parasites).
Si hayo tu bali kitunguu saumu kinaendelea kuleta maajab katika miili
ya binadam na huweza kufanya yafuatayo pia: Uweo wa kulainisha na
kuondoa gesi, kutibu vidonda katika ngozi, huhifadhi maji. Vumbi la
kitunguu saumu likichanganywa na asli akipakwa mwenye ukoma litamfaa,
kitunguu saumu humfaa mwenye maradhi magonjwa ya mishipa na nyonga
(sciatia). Maji yake (yaliotolewa kwa kupikwa) hutuliza maumivu ya meno,
si hayo tu bali vilevile hufaa kwa kikohozi.
Kitunguu saumu
kimekusanya protein 49% mafuta muhimu ya sulphur 25% na kiasi flani cha
chumvi, homoni (hormones) zitiazo nguvu za kiume na vinavyoteremsha
hedhi.
BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU SAUMU:
Kiuasumu:
Saga tembe tano za kitunguu saumu, changanya na asali kikombe kimoja
kilichochanganywa na habbasouda na kunywa papo hapo. Kunywa asubuhi na
jioni. Paka mafuta ya kitunguu saumu pahala panapouma iwapo ni sumu ya
nyoka au paka nje ya tumbo iwapo umekunywa sumu.
Kusafisha tumbo:
Kabla ya kula chakula, meza tembe za kitunguu saumu na baadae kunywa
maji ya shimari yaliyochanganywa na asali kwa muda wa wiki moja.
Kiyeyusha mafuta (Cholestrol):
Unapokula chakula kila siku, weka katika kachumbari kiasi cha tembe 2 vilivyosagwa ule pamoja na kachumbari.
Kiongeza mkojo chenye kusafisha njia za mkojo:
Chemsha vizuri hairi, na baada ya kupoa tia tembe 3 za kitunguu
saumu zilizosagwa. Kunywa kinywaji hicho kila siku kabla ya kula na
kunywa juisi ya limau/ndimu.
Kuharisha damu (Dysentery):
Chukua tembe ya kitunguu saumu uikatekate na uile; fanya hivyo kwa muda
wa wiki moja na bora zaidi ukinywa na mafuta ya zaituni kijiko kimoja.
Gesi na Indegestion:
Kunywa juisi ya pea iliyochanganywa na tembe 3 za kitunguu saumu kabla ya kulala kila siku.
Kutibu Typhoid:
Kata tembe 5 za kitunguu saumu, changanya ndani ya maziwa ya moto
yaliyochanganywa na asali kunywa kabla ya kulala. Pia paka uti wa mgongo
mafuta ya kitunguu saumu yaliyochanganywa na mafuta ya zeti, na asubuhi
vuta moshi wa kitunguu saumu kwa muda wa dakika 5.
Kidonda kilichooza:
Ponda kitunguu saumu mpaka iwe laini kama marhamu halafu jifunge nacho
kwa kutumia bendeji, japo kitawasha lakini kitazuia ugonjwa wa gangrene
ambao unaweza ukapelekesha kukatwa kiungo. Vilevile unaweza kusafisha
kidonda kwa kuchanganya kitunguu saumu kilichosagwa kikatiwa maji
vuguvugu (warm water) na kikasafishwa kidonda.
Mishipa:
Kata tembe za kitunguu saumu na umeza kwa maziwa ya moto (sio moto sana)
yenye matone ya ambari kabla ya kulala kila siku, dawa hii huipa
mishipa nguvu.
Homa ya mafua (Influenza):
Kunywa juisi ya machungwa na juisi ya limau zilizochanganywa na tembe 7
za kitunguu saumu kunywa juisi hiyo kabla ya kulala. Vuta moshi wa
kitnguu saumu.
Mafua:
Meza tembe za kitunguu thaum baada ya chakula pamoja na juisi ya
kitunguu saumu iliyochanganywa na juisi ya limau pamoja na kuvuta moshi
wa kitunguu saumu.
Saratani (Cancer):
Katika kitunguu saumu kuna kiini kinachozuia saratani, kwa kila mgonjwa
wa saratani anashauriwa ale kwa wingi kitunguu saumu na karoti (carrot).
Kifua kikuu (cha mapafu):
Kila asubuhi kabla ya kula chakula meza tembe 3 za kitunguu saumu, saga ule pamoja na mkate na jioni vuta moshi wake.
Kipindupindu (cholera):
Ili kujikinga na maradhi hayo wakati kikienea, kula kijiko kimoja cha
kitunguu saumu kilichosagwa na kukorogewa katika asali baada ya kila
chakula.
Kutoa minyoo:
Ponda tembe 3 za kitunguu saumu, tia ndnai ya maziwa na kunywa (bila
kutia sukari) jioni kabla ya kulala na asubuhi kunywa mafuta ya mbono.
Upele:
Chukua tembe 5 za vitunguu saumu uvisage na uvikoroge katika shahamu na
paka pale penye upele kuazia jioni mpaka asubuhi na ukoshe kwa maji ya
moto tumia kwa muda wa wiki moja.
Mbaa kichwani:
Ponda uzuri vitunguu saumu 3 na uvikoroge katika siki ya tofaha (Apple
vinegar) katika chupa ya bilauri (sio plastiki) na uache juani kwa muda
wa wili moja. Baada ya hapo jipake kichwani pamoja na kusugua kwa muda
wa wili 1 na baada ya wiki jipake mafuta ya zeituni.
Nguvu za kiume:
Saga kitunguu saumu kitie ndani ya mafuta ya zeti na weka katika moto
mdogo mdogo mpaka iwe rangi ya manjano na tia katika chupa na wakati wa
haja jipake katika dhakari na osha baada ya saa moja.
Kujenga misuli na kutia nguvu:
Kila siku kabla ya kula kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia
yaliyotiwa tembe 2 za kitunguu saumu iliyosagwa. Kunywa kwa muda wa
mwezi mmoja mfululizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni