Ikiwa imebakia mienzi miwili na siku kadhaa kwa
visiwa vya Unguja na Pemba (Zanzibar) kufikia kilele cha maadhimisho ya
kusherehekea mapindizi matukufu, serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imemua
kuadhimisha sherehe hizo za miaka 50 tangia kuingia madarakani kwake kwa ustadi
mkubwa sana.
Miongoni mwa vitu vinavyofanya sherehe hizo kuwa za
aina yake ni ujenzi wa Mnara mkubwa katika Mji wa Zanzibar, utakaojengwa maeneo
ya Michenzani katika kisiwa cha Unguja.
picture ikionesha hali halisi itakavyokua baada ya ujenzi wa mnara huo kukamilika.
Mnara huo unasadikika kutumia kiasi cha Shilingi
Billion Moja mpaka kukamilika kwake, huku ukitabiriwa kuwa ni kivutio kikubwa
huko mbeleni kwa biashara ya Utalii. Mbali na Mnara huo miradi mingi
imekamilika na kutarajiwa kufunguliwa na viongozi kadhaa wa Kitaifa, kama vile
Shule, Usambazaji wa miundombinu barabara mijini na vijijini, na pamoja na
upatikanaji wa maji safi na yenye uhakika katika maeneo yote ya Zanzibar.
picture ikionesha hali halisi ya ujenzi wa mnara ikiendelea.
Hongera miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar na karibu
Mnara mpya utakao nasibisha mazingira ya Zanzibar kitaifa na Kimataifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni