Jumamosi, 30 Novemba 2013

MAAMBUKIZO YA UKIMWI YAONGEZEKA ZANZIBAR:


Zanzibar,
Mkurugenzi Mtendaji wa Kamishina ya Ukimwi Zanzibar (ZAC) Dk. Omar Shauri Makame amesema kwamba RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein atakuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yatakayofanyika Paje Mkoa wa Kusini Unguja .

Akitoa taarifa hiyo, Dk. Makame amesema maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika wakati kunaonekana kuwapo na ongezeko la maambukizi mapya.

Alisema katika mwaka 2012-2013 watu 108 walikutwa na maambukizi mapya na kufanya idadi ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi kufikia 6,125 kwa mujibu wa takwimu za watu waliofika katika vituo vya afya kuchunguza afya zao ikiwemo damu.

“Utafiti wa takwimu za ugonjwa wa Ukimwi zinaonesha kwamba yapo maambukizi mapya ya ugonjwa huo kwa kiwango kikubwa ambapo juhudi za makusudi zinahitajika.

“Kwa mfano alisema Tume ya Ukimwi imeweka mikakati kuyadhibiti makundi hatarishi ikiwemo vijana wanaotumia dawa za kulevya ambapo maambukizi ya kundi hilo yapo kwa asilimia 25’” alisema Dk. Makame.


Picha ni Ramani ya kisiwa cha Zanzibar ambacho ni maarufu kwa jina la marashi ya Karafuu.

HUKUMU YA UJENZI YA JENGO LA GHOROFA 18 KARIBU NA IKULU DAR ES SALAAM

Picha inayoonesha mandhari yote ya hali ilivyo kwa sasa.


Awali akijitetea Maliyaga alidai kuwa, Mkurugenzi wa Miliki wa Wakala, Charles Makungu ndiye aliyekuwa na uamuzi wa mwisho wa kutoa kibali cha ujenzi na kupeleka barua katika halmashauri husika na kwa waleta maombi.

Akiongozwa na Wakili Majura Magafu, Maliyaga alidai alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kutoa Vibali na walipopata ombi la ujenzi huo walipitia michoro na baada ya kuona ipo sawa alisaini kibali na kupeleka kwa Makungu.


Alidai kuwa awali aliandika barua akipendekeza ofisi ya Makungu iombe kibali kutoka Halmashauri ya Ilala lakini hakupata majibu hadi alipopewa maelekezo kutoka katika kamati inayoshughulikia miradi ubia kuwa watoe kibali hicho. Alidai alikataa kutoa kibali hicho lakini baada ya wanakamati kujadili walikubali kufuata maelekezo hayo na kutoa kibali hicho.


"Sisi hatukuhusika katika kutoa uamuzi wa mradi huu, mimi nimeonewa kwasababu sijanufaika na sikutumia madaraka yangu vibaya na nashangaa kwanini Makungu, watu kutoka katika kamati yetu au ile ya miradi ya ubia hawajaletwa mahakamani," alidai Maliyaga.


Katika utetezi wake hivi karibuni Kimweri alidai kuwa amefunguliwa kesi hiyo kwa kuwa alikuwa na ugomvi na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli baada ya kumchafua kwenye vyombo vya habari.


Alidai ugomvi huo ulitokana na mchakato wa uuzwaji wa nyumba za Serikali ambapo yeye alikataa kusaini mkataba wa kumuuzia nyumba mwanafunzi kwa sababu hakustahili ndipo Magufuli alipodhani kuwa alitoa taarifa hizo kwenye vyombo vya habari.


Kimweri na Maliyaga wanakabiliwa na mashitaka matano ya matumizi mabaya ya ofisi katika utoaji kibali cha ujenzi wa jengo la ghorofa 15 kiwanja namba 45 mtaa wa Chimara.


Aidha wanadaiwa kutoa kibali kingine cha kuongeza ujenzi kutoka ghorofa 15 hadi 18.

Picha halisi inayoonesha muonekano wa Jengo lenyewe lenye Utata.


Picha inayoonesha hali halisi ya muonekano wa Ikulu pindi unapokuwepo juu ya jumba hilo.



Ijumaa, 29 Novemba 2013

TUME YA KATIBA YAONGEZEWA WIKI MBILI:



Rais Jakaya Kikwete ameiongezea tena muda Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili kuiwezesha kumaliza kazi yake.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu juzi usiku, ilisema Rais Kikwete ameiongezea siku 14.
Tume hiyo ambayo ilitakiwa kumaliza kazi yake, Desemba 15, mwaka huu itaendelea na kazi kuanzia Desemba 16 hadi Desemba 30, mwaka huu.
Hii ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kuiongezea Tume hiyo muda wa kufanya kazi yake. Baada ya maombi yake ya kwanza, Rais Kikwete aliiongezea Tume hiyo siku 45 kuanzia Novemba Mosi hadi Desemba 15, mwaka huu.
Kabla ya kuomba kuongezewa muda, ilitakiwa kukamilisha kazi yake kesho.
Rais Kikwete ameiongezea Tume hiyo muda zaidi kwa mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 8(3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inaelekeza Tume hiyo kufanya kazi kwa miezi 18 licha ya kuwa sheria inampa Rais mamlaka ya kuiongezea tume hiyo muda wa kufanya kazi usiozidi siku 60.
Kwa uamuzi wake, wa kuiongezea Tume hiyo siku nyingine 14, Rais Kikwete atakuwa ameiongezea tume hiyo jumla ya siku 59 kati ya 60 ambazo anaruhusiwa kisheria.
Hatua hiyo ilitarajiwa hasa baada ya Tume hiyo kusimamisha kazi zake kwa muda baada ya kifo cha mmoja wa wajumbe wake, Dk Sengondo Mvungi kilichotokea Novemba 12, mwaka huu nchini Afrika Kusini alikokuwa anatibiwa baada ya kujeruhiwa kwa mapanga na watu wasiojulikana nyumbani kwake Novemba 3, mwaka huu.
Baada ya kifo hicho, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba alitangaza kusitishwa kwa muda shughuli za Tume hiyo.
Kifo cha Dk Mvungi, ambaye aliteuliwa kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi kilikuwa pigo kwa Tume hiyo kwani mwanasheria huyo alikuwa amebobea katika masuala ya katiba.
Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 3, 2012 kwa kukusanya maoni ya wananchi, iliandaa rasimu ya kwanza iliyotolewa Juni 4, mwaka huu.


Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania. Mh. Dr Jakaya Mrisho Kikwete.




WATANZANIA WAKAMATWA AFRIKA KUSINI NA MADAWA YA KULEVYA:



Watanzania wawili wanahojiwa na Polisi wa Afrika Kusini baada ya kukamatwa jana na kilo 55 za dawa za kulevya.

Watu hao wawili wanatazamiwa kufikishwa mahakamani kesho kujibu tuhuma za kukamatwa na dawa hizo zenye thamani ya Rand75 milioni (Sh11.7 bilioni).

Maofisa wa Kikosi Maalumu cha Kupambana na Makosa ya Jinai na Rushwa cha Afrika Kusini (The Hawks), kiliwakamata watu hao katika Kitongoji cha Kempton Park, Ekurhuleni, Jimbo la Gauteng.

Msemaji wa Hawks, Paul Ramaloko alisema jana kuwa maofisa hao walivamia nyumba waliyokuwa wanaishi Watanzania hao na kukuta mzigo huo.

Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya watu hao kwa kuhofia kuharibu uchunguzi akisema bado walikuwa wanawasaka watuhumiwa zaidi wakiwamo raia wa Afrika Kusini.

Alisema kikosi chao kimepata mafanikio makubwa kwa kukamata dawa nyingi kiasi hicho…



Jumanne, 26 Novemba 2013

UJERUMANI YAPIGA MKWARA VIONGOZI WAKE WOT WA JUU KUTUMIA VIFAA VYA APPLE


Shirika la Apple lina makubaliano ya siri na Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani NSA yanayoruhusu mawasiliano yote ya simu za iPhone na data za simu hizo pamoja na vifaa vingine vya Apple zikiwemo kompyuta zipitishwe kwenye chujio linalowasilisha taarifa zake moja kwa moja kwa wakala huo wa kijasusi wa Marekani.


Ujerumani imeamrisha Viongozi wake wote wa ngazi ja juu kutotumia vifaa vyote vya Apple zikiwamo computers.

Jumapili, 24 Novemba 2013

Dkt. MALIK AJERUHIWA JIJINI NAIROBI



Mkurugenzi Mkuu wa wizara ya afya Zanzibar na  Daktari Bingwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, amelazwa katika hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi baada ya kujeruhiwa vibaya na majambazi.
Dkt. Malik alikuwa Nairobi kikazi na alipotea tangu Ijumaa iliyopita na hakukuwa na mawasiliano nae, wahusika wa hoteli aliyofikia pia hawakuwa wakifahamu alipo mgeni wao.


Alhamisi, 21 Novemba 2013

KITUNGUU SAUMU NA MAAJABU YAKE.

Kitunguu saumu kina harufu ya pekee isiyowapendeza watu wengi, ila kina uwezo wa kutibu magonjwa lukuki ambayo na imani hukulijua hilo. Katika nyakati hizi dunia yetu imezungukwa na magonjwa mengi ya maambukizi na ya sio maambukizi kama mifupa, uchovu wa mwili na kadhalika.

Imethibitishwa kisayansi kuwa kitunguu saumu husafisha damu kutokana na mafuta (cholestrol) ambayo husababisha magonjwa ya mishipa ya ateri na maradhi ya moyo, na pia husafisha damu kutokana na vijidudu na maikrobati kuliko (antibiotic) vengine. Sio hivyo tu bali kitunguu saumu kimethibitika kuwa na uwezo wa kuzuia kuenea kwa sumu ya nyoka katika mwili wa binadamu na husafisha maida kutokana na vimelea (parasites).

Si hayo tu bali kitunguu saumu kinaendelea kuleta maajab katika miili ya binadam na huweza kufanya yafuatayo pia: Uweo wa kulainisha na kuondoa gesi, kutibu vidonda katika ngozi, huhifadhi maji. Vumbi la kitunguu saumu likichanganywa na asli akipakwa mwenye ukoma litamfaa, kitunguu saumu humfaa mwenye maradhi magonjwa ya mishipa na nyonga (sciatia). Maji yake (yaliotolewa kwa kupikwa) hutuliza maumivu ya meno, si hayo tu bali vilevile hufaa kwa kikohozi.

Kitunguu saumu kimekusanya protein 49% mafuta muhimu ya sulphur 25% na kiasi flani cha chumvi, homoni (hormones) zitiazo nguvu za kiume na vinavyoteremsha hedhi.




BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU SAUMU:

Kiuasumu:
Saga tembe tano za kitunguu saumu, changanya na asali kikombe kimoja kilichochanganywa na habbasouda na kunywa papo hapo. Kunywa asubuhi na jioni. Paka mafuta ya kitunguu saumu pahala panapouma iwapo ni sumu ya nyoka au paka nje ya tumbo iwapo umekunywa sumu.



Kusafisha tumbo:
Kabla ya kula chakula, meza tembe za kitunguu saumu na baadae kunywa maji ya shimari yaliyochanganywa na asali kwa muda wa wiki moja.

Kiyeyusha mafuta (Cholestrol):
Unapokula chakula kila siku, weka katika kachumbari kiasi cha tembe 2 vilivyosagwa ule pamoja na kachumbari.

Kiongeza mkojo chenye kusafisha njia za mkojo:
Chemsha vizuri hairi, na baada ya kupoa tia tembe 3 za kitunguu saumu zilizosagwa. Kunywa kinywaji hicho kila siku kabla ya kula na kunywa juisi ya limau/ndimu.

Kuharisha damu (Dysentery):
Chukua tembe ya kitunguu saumu uikatekate na uile; fanya hivyo kwa muda wa wiki moja na bora zaidi ukinywa na mafuta ya zaituni kijiko kimoja.

Gesi na Indegestion:
Kunywa juisi ya pea iliyochanganywa na tembe 3 za kitunguu saumu kabla ya kulala kila siku.

Kutibu Typhoid:
Kata tembe 5 za kitunguu saumu, changanya ndani ya maziwa ya moto yaliyochanganywa na asali kunywa kabla ya kulala. Pia paka uti wa mgongo mafuta ya kitunguu saumu yaliyochanganywa na mafuta ya zeti, na asubuhi vuta moshi wa kitunguu saumu kwa muda wa dakika 5.

Kidonda kilichooza:
Ponda kitunguu saumu mpaka iwe laini kama marhamu halafu jifunge nacho kwa kutumia bendeji, japo kitawasha lakini kitazuia ugonjwa wa gangrene ambao unaweza ukapelekesha kukatwa kiungo. Vilevile unaweza kusafisha kidonda kwa kuchanganya kitunguu saumu kilichosagwa kikatiwa maji vuguvugu (warm water) na kikasafishwa kidonda.

Mishipa:
Kata tembe za kitunguu saumu na umeza kwa maziwa ya moto (sio moto sana) yenye matone ya ambari kabla ya kulala kila siku, dawa hii huipa mishipa nguvu.

Homa ya mafua (Influenza):
Kunywa juisi ya machungwa na juisi ya limau zilizochanganywa na tembe 7 za kitunguu saumu kunywa juisi hiyo kabla ya kulala. Vuta moshi wa kitnguu saumu.

Mafua:
Meza tembe za kitunguu thaum baada ya chakula pamoja na juisi ya kitunguu saumu iliyochanganywa na juisi ya limau pamoja na kuvuta moshi wa kitunguu saumu.

Saratani (Cancer):
Katika kitunguu saumu kuna kiini kinachozuia saratani, kwa kila mgonjwa wa saratani anashauriwa ale kwa wingi kitunguu saumu na karoti (carrot).

Kifua kikuu (cha mapafu):
Kila asubuhi kabla ya kula chakula meza tembe 3 za kitunguu saumu, saga ule pamoja na mkate na jioni vuta moshi wake.

Kipindupindu (cholera):
Ili kujikinga na maradhi hayo wakati kikienea, kula kijiko kimoja cha kitunguu saumu kilichosagwa na kukorogewa katika asali baada ya kila chakula.

Kutoa minyoo:
Ponda tembe 3 za kitunguu saumu, tia ndnai ya maziwa na kunywa (bila kutia sukari) jioni kabla ya kulala na asubuhi kunywa mafuta ya mbono.

Upele:
Chukua tembe 5 za vitunguu saumu uvisage na uvikoroge katika shahamu na paka pale penye upele kuazia jioni mpaka asubuhi na ukoshe kwa maji ya moto tumia kwa muda wa wiki moja.

Mbaa kichwani:
Ponda uzuri vitunguu saumu 3 na uvikoroge katika siki ya tofaha (Apple vinegar) katika chupa ya bilauri (sio plastiki) na uache juani kwa muda wa wili moja. Baada ya hapo jipake kichwani pamoja na kusugua kwa muda wa wili 1 na baada ya wiki jipake mafuta ya zeituni.

Nguvu za kiume:
Saga kitunguu saumu kitie ndani ya mafuta ya zeti na weka katika moto mdogo mdogo mpaka iwe rangi ya manjano na tia katika chupa na wakati wa haja jipake katika dhakari na osha baada ya saa moja.

Kujenga misuli na kutia nguvu:
Kila siku kabla ya kula kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia yaliyotiwa tembe 2 za kitunguu saumu iliyosagwa. Kunywa kwa muda wa mwezi mmoja mfululizo.

WAWILI WAIAGA DUNIA WAKIOGELEA DAR.


Dar es Salaam. Watu watu wawili waliokuwa wakiogelea ufukweni mwa Bahari ya Hindi kuzama na kufa baada ya kuzidiwa na nguvu ya maji.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Ndugu Kiondo alisema mnamo Novemba 17 mwaka huu saa 11.30 jioni eneo la Ufukwe wa Ng’onda Kata ya Kigamboni, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Miembeni Vingunguti, Hajira Juma (11) akiwa na watoto kutoka kituo cha yatima Orphans wakiwa wanaogelea, maji yalimzidi nguvu na kuzama.

Kiondo alisema watoto wa kutoka kituo hicho walimtafuta ilipofika saa 12.15 jioni maiti yake ilionekana kandokando mwa bahari hiyo.

Kiondo alisema Chanzo cha kifo chake inasadikiwa ni kutokuwa na ujuzi wa kuogelea na maiti imehifadhiwa Hospitali ya Vijibweni.


ASKARI WA MISRI WASHAMBULIWA SINAI.


Askari kumi wa Misri wameripotiwa kuuawa na wengi kujeruhiwa kutokana na kulipuliwa na bomu karibu na mji wa el-Arish kaskazini mwa Sinai nchini Misri.

Gazeti la Al-Masri al-Youm limesema msafara wa mabasi yakiwa yamebeba askari wa miguu ulipigwa na bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara wakati msafara huo ukielekea katika eneo la Kharouba.

Mashambulio dhidi ya askari wa usalama katika eneo la Sinai, kaskazini mwa Misri yameongezeka tangu Rais Mohammed Morsi ang'olewe madarakani mwezi Julai mwaka huu.

Hali ya usalama katika eneo hilo imezidi kuzorota katika miaka ya karibuni, ikichochewa na kuangushwa kwa Rais Hosni Mubarak. Kuondolewa kwake madarakani mwezi Februari 2011 kulisababisha eneo la kaskazini mwa Sinai kulengwa na vikundi vya wapiganaji, vikundi vingine vikihusishwa na wapiganaji wa ukanda wa Gaza, huko Palestina.

DRC YASEMA UGANDA INA MASLAHI BINAFSI NA WAASI WA M23


Hatua ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kukataa kusaini mkataba wa amani na kundi la waasi la M23, imepeleka kilio kwa kundi hilo, na sasa wanashindwa kuelewa hatima yao nchini Uganda.

Uganda, nchi ambayo ni msuluhishi wa mgogoro huo baina ya DRC na waasi wa M23, imejikuta katika wakati mgumu kwani kundi la waasi wa M23 wapatao 1,700.

Msemaji wa Serikali ya DRC, Lambert Mende, mwishoni mwa wiki ametamka kuwa “Serikali ya DRC ina wasiwasi kuwa Uganda ambayo kwa sasa inaonekana kuwa sehemu ya mgogoro na imeshindwa kuficha maslahi yake binafsi na waasi wa M23. Kwa sababu hiyo hatuko tayari kutia saini mkataba unaosimamiwa kwa mitego.”

Kauli hii ya Mende imekuja siku chache baada ya DRC kukataa kutiliana saini na waasi kwa maelezo kuwa M23 ni kundi lililotangaza kujivunja, wamekimbilia Rwanda na Uganda, na hivyo kulipa sharti kubwa wanalolikataa.



Sharti hilo ni kuwa mkataba uwe na kipengele kinachowazuia M23 milele kutoshika silaha na kuanzisha mapambano, hoja inayokataliwa na waasi, huku Uganda ikizishawishi pande mbili zitie saini mkataba hivyo hivyo ulivyo kwa maelezo kuwa yakitokea matatizo mbele ya safari utarekebishwa tena.


Masharti mengine wanayowapa waasi hao ni kuwa makamanda wapatao 100 waliokuwa wanaongoza kundi la M23, wasiruhusiwe kuingia jeshini moja kwa moja, na badala yake wapewe mafunzo ya kijeshi, huku wakiacha fursa ya kushitaki wahalifu wa kivita watakaothibitika mbele ya safari kuwa walitenda uhalifu dhidi ya binadamu.

Uganda pia imetishia kwa mara nyingine mwishoni mwa wiki kuwa ikiwa suluhu haitapatikana haraka, na DRC ikaendelea kuituhumu kuwa inashirikiana na waasi wa M23, basi yenyewe itajitoa katika nafasi ya kuwa msuluhishi.

Jumanne, 19 Novemba 2013

ZANZIBAR KUYAENZI MAPINDUZI KWA STYLE YA AINA YAKE.


Ikiwa imebakia mienzi miwili na siku kadhaa kwa visiwa vya Unguja na Pemba (Zanzibar) kufikia kilele cha maadhimisho ya kusherehekea mapindizi matukufu, serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imemua kuadhimisha sherehe hizo za miaka 50 tangia kuingia madarakani kwake kwa ustadi mkubwa sana.
Miongoni mwa vitu vinavyofanya sherehe hizo kuwa za aina yake ni ujenzi wa Mnara mkubwa katika Mji wa Zanzibar, utakaojengwa maeneo ya Michenzani katika kisiwa cha Unguja.

picture ikionesha hali halisi itakavyokua baada ya ujenzi wa mnara huo kukamilika.

Mnara huo unasadikika kutumia kiasi cha Shilingi Billion Moja mpaka kukamilika kwake, huku ukitabiriwa kuwa ni kivutio kikubwa huko mbeleni kwa biashara ya Utalii. Mbali na Mnara huo miradi mingi imekamilika na kutarajiwa kufunguliwa na viongozi kadhaa wa Kitaifa, kama vile Shule, Usambazaji wa miundombinu barabara mijini na vijijini, na pamoja na upatikanaji wa maji safi na yenye uhakika katika maeneo yote ya Zanzibar.

picture ikionesha hali halisi ya ujenzi wa mnara ikiendelea.

Hongera miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar na karibu Mnara mpya utakao nasibisha mazingira ya Zanzibar kitaifa na Kimataifa.

CHINA NA BIASHARA YA PEMBE ZA NDOVU


China imekuwa soko kubwa la pembe za ndovu kuanzia mwaka 2009, kabla ya hapo soko kubwa lilikuwa Japan na nchi nyingine za Asia kusini mashariki.
- Nchini China, pembe za ndovu na na bei zake ni kubwa, mfano kinyago kilichotengenezwa meno nzima kinauzwa kwa Yuan milioni 1.7, sawa na dola elfu 280 za kimarekani!

Raia wa China wakiwa pamoja na pembe za Ndovu katika Stock yao nchini Tanzania


Waziri Khamis Kagasheki akinena na Raia wa China baada ya kugundulika  kuhifadhi Pembe za Ndovu katika stock yao.

MAHAFALI: UDSM


Wahitimu wa Shahada na Stashahada mbalimbali kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, wakiwa kwenye mahafali ya 43 ya chuo hicho jijini Dar es Salaam juzi. sherehe hizo ilifanyika kwa ustadi mkubwa huku wahitimu wa mahafali hayo wakijumuika na familia zao ilikuweza kupata baraka za pamoja miongoni mwao.





Uongozi wa blog hii unawapongeza wahitimu wote waliohitimu chuoni hapo, na kuweza kuwa ndio chachu ya mafanikio katika kulijenga na kulilinda Taifa letu.

HILI NDILO HITIMISHO LA DR SENGONDO MVUNGI.


Aliekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Nchini Dr. sengondo Mvungi, amezikwa leo Kijijini kwake wilaya ya Mwanga, Mkoani Kilimanjaro.



HIZI NDIZO PICHA ZA HOTELI YA MAJABU ILIYOKO CHINI YA MAJI ZANZIBAR


Manta Resort” Hotel hii ya kipekee iliyoko visiwani Zanzibar yawa gumzo kwenye Vyombo vya Habari vya ulimwenguni...

Ina vyumba chini ya maji na Bei ya kulala kwa siku ni $900 single na a$1,500 double..Hoteli imekua gumzo kwenye vyombo vya habari vya kimataifa na ndio hoteli pekee yenye vyumba vya chini ya maji Barani Africa ambapo mtu akiwa chumbani anaweza kuona samaki wakipita nje ya dirisha lake…Tazama picha zaidi hapa chini,,,,




hakuna kinachoshindikana ni katika ulimwengu huu hizi ni baadhi ya picha za hoteli mpya tu inayopatikana hapa dunia, jee unahisi inapatikana katika maeneo gain hapa ulimwenguni??
Jibu lake ni rahi tu, iko huko Zanzibar kwenye kisiwa pacha cha Unguja, hapa namaanisha ni kisiwa cha Pemba.
Hotel hiyo imezinduliwa mwezi huu yenye vyumba 16 ijulikanayo kwa jina la The Manta Resort ikiwa designed by Swedish company Genberg Underwater Hotels kwa mujibu wa chanzo cha CNN.

Yani ukiwa umelala chumbani unaona samaki kabisa kupitia madirisha ambapo gharama yake kulala kwa watu wawili ni dola za Kimarekani 1500 ambayo ni zaidi ya milioni mbili za kitanzania na kwa mtu mmoja ni $900 ambayo inagonga kwenye milioni moja na laki nne hivi.