Dar es Salaam. Watu watu wawili waliokuwa wakiogelea
ufukweni mwa Bahari ya Hindi kuzama na kufa baada ya kuzidiwa na nguvu
ya maji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Ndugu Kiondo
alisema mnamo Novemba 17 mwaka huu saa 11.30 jioni eneo la Ufukwe wa Ng’onda
Kata ya Kigamboni, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Miembeni Vingunguti,
Hajira Juma (11) akiwa na watoto kutoka kituo cha yatima Orphans wakiwa
wanaogelea, maji yalimzidi nguvu na kuzama.
Kiondo alisema watoto wa kutoka kituo hicho
walimtafuta ilipofika saa 12.15 jioni maiti yake ilionekana kandokando
mwa bahari hiyo.
Kiondo alisema Chanzo cha kifo chake inasadikiwa ni kutokuwa na ujuzi wa kuogelea na maiti imehifadhiwa Hospitali ya Vijibweni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni